Thursday 12 March 2015

ELIMU KWA JAMII JUU YA AINA ZA WAGANGA

Katika swala la utoaji elimu kwa Jamii, elimu juu ya Tiba Asili inafaa itolewe na Waganga wa Asili wenyewe ili kuweza kubadilisha Imani zinazowapotosha wanajamii hata kufikia kutendeana maovu yanayopelekea mauaji. Elimu hii si vyema ikatolewa na Watu wengine kama Vile Maaskofu, Masheikh, Wanasheria, Madaktari wa Kisasa, Wanasiasa n.k kwa kuwa Jamii haitapokea ujumbe wao Kirahisi kwani wamezoeleka kwa Kazi zingine siyo kwa Kazi hiyo ya Imani za ushirikina na uchawi
Katika Imani ya kawaida Kuna Aina za waganga kama ifuatavyo
                              I.            Waganga wa Asili
                           II.            Waganga wa Jadi
                        III.            Waganga wa Kienyeji

1.    WAGANGA WA ASILI.
Mganga wa Asili ni yule anayeshughurika na Tiba za Maradhi kwa Kutumia dawa zaAsili ili kuondoa Maradhi yanayosumbua Jamii iwe kwa Binadamu, wanyama, mimea n.k kwa Kufuata maadili ya utoaji huduma ya Utabibu

2.    WAGANGA WA JADI.
Mganga wa Jadi ni yule anaetumia Mila na Desturi katika Tiba na Utoaji wa dawa kwa wagonjwa iwe Binadamu, Wanyama, Mimea n.k. hivyo hutegemea Zaidi Mila na Desturi kama kanuni na maadili ya utoaji wa Huduma ya Tiba.

3.    MGANGA WA KIENYEJI.
Mganga wa Kienyeji ni Yule Ambaye hana Mafunzo Maalum ya Tiba ya Upande wowote maalum wa tiba  ya Upande wowote katika utoaji wake huduma kwa jamii. Ni mtu anayeweza kuchanganya taaluma mbalimbali hata za kisayansi ili mradi afanikishe alichokusudia. Mganga huyo pia anaweza kutumia vazi lolote liwe la sheikh, askofu, daktari, Mganga wa asili n.k ili mradi atimize alokusudia. Mganga yeyote mwenye fani nzuri akiitumia katika kutenda maovu hufahamika kama mganga wa Kienyeji katika Tiba za Asili.

je Huyu ni Aina gani ya Mganga?

0 comments:

Post a Comment

NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA

Flag Counter

Text Widget