Friday, 20 March 2015

TFDA YATEKETEZA BIDHAA FEKI ZENYE THAMANI YA SH MIL.5, SIKONGE MKOANI TABORA


Baadhi ya bidhaa zilizoteketezwa na Maofisa wakaguzi wa TFDA wilayani Sikonge.
Maofisa wakaguzi wa TFDA kanda ya kati wakijiandaa kuteketeza bidhaa zilizoisha mda wake ikiwemo vinywaji wilayani Sikonge (picha na Allan Ntana).

Na Allan Ntana, Sikonge

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati imefanikiwa kukamata na kuteketeza bidhaa mbalimbali za chakula, vinywaji, dawa za binadamu na mifugo, vipodozi na vifaa tiba vilivyoisha muda wake na vingine feki vyenye thamani ya zaidi ya sh mil.5 katika halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Akisoma taarifa ya ukaguzi mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo hapo juzi Afisa Mkaguzi wa Chakula Kanda ya Kati Sifa Chamgenzi alisema ukaguzi huo ulilenga kuangalia ubora na usalama wa dawa za binadamu na mifugo, uwepo wa vipodozi vilivyopigwa marufuku na bidhaa zingine zilizoisha muda wake wa matumizi. 

Alisema lengo la TFDA ni kufuatilia utekelezaji wa sheria na.1 ya mwaka 2003 ya chakula, dawa na vipodozi kwa wauzaji na wasindikaji wa vyakula na dawa na kuongeza kuwa zoezi hili lililenga kutekeleza mpango kazi wa Mamlaka hiyo wa kufuatilia ubora na usalama wa bidhaa hizo kwa mtumiaji.

Ukaguzi huo uliofanyika tarehe 20-29 Januari 2015 uliongozwa na Maafisa wakaguzi wawili kutoka TFDA Kanda ya Kati Fredrick Luyangi na Sifa Chamgenzi ambao waliungana na wakaguzi wenyeji wawili toka Ofisi ya Mkurugenzi Idara ya Afya na askari polisi wanne wilayani Sikonge na jumla ya majengo 118 yanayojihusisha na biashara ya chakula, vinywaji, dawa, vipodozi na vifaatiba yalikaguliwa.

Katika ukaguzi huo baadhi ya maduka yalikamatwa na vipodozi vilivyopigwa marufuku vikiwa na uzito wa kilo 164.4 na thamani ya sh 1,856,000/- na katika maduka ya vyakula walikamata vyakula vilivyoisha muda wake vyenye uzito wa kilo 825.5 vikiwa na thamani ya sh 2,720,000/-

Na katika maduka ya dawa za binadamu na mifugo walikamata jumla ya kilo 37 za dawa zilizoisha mda wake na feki zenye thamani ya sh 1,200,000/-.

Aidha katika ukaguzi huo kiasi cha sh 1,580,000 kilipatikana kutokana na ada za usajili wa maduka ya biashara ya chakula ambapo 40%  ya kiasi hicho sawa na sh 632,000 inabakia katika halmashauri kwa ajili ya kufanya kazi za TFDA.

Akizungumzia mambo waliyoyabaini wakati wa ukaguzi huo, Chamgenzi alisema ukaidi na uelewa mdogo wa sheria na.1 ya mwaka 2003 wa kulipa ada na tozo husika kwa baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya chakula, dawa na vipodozi bado ni tatizo sambamba na kutotoa ushirikiano kwa Afisa wakaguzi.

Aidha uwepo wa dawa bandia (feki) zilizoondolewa sokoni, dawa na vyakula vilivyoisha muda wake, kukosekana feni za kutunzia dawa katika stoo ya kituo cha afya Kitunda, maduka ya dawa za kilimo kuuza dawa za mifugo kinyume cha sheria, utunzaji mbovu na mlundikano wa dawa zilizoisha muda wake, viwanda na mashine za unga kuwa katika makazi ya watu ni miongoni mwa yaliyobainika.

Wakaguzi hao pia hawakuridhishwa na hali ya machinjio ya halmashauri hiyo kukosa uzio, kutokuwa na chanzo cha maji cha kuaminika na sakafu kuwa na mashimomashimo hali iliyosababisha kutuama kwa maji na damu na hivyo kuhatarisha afya za walaji, hivyo wakamwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo Shadrack Mhagama kufanyia kazi mapungufu hayo kwani yanarekebika, jambo ambalo aliliafiki na kuahidi kutekeleza mara moja.

MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA SHEREHE YA KUTIMIZA MWAKA VIKUNDI VYA WAMA HUKO NACHINGWEA/ AKABIDHI MADAWATI

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Nachingwea kuhudhuria sherehe za kutimiza mwaka za vikundi vya WAMA kwenye Mradi wa Mwanamke Mwezeshe tarehe 18.3.2015.
2Mamia ya wanavikundi na viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za kutimiza mwaka za vikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe katika Mkoa wa Lindi zilizofanyika Nachingwea wakifuatilia kwa makini sherehe hiyo.
3 4Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaonyesha waalikwa zawadi mbalimbali alizopewa na wanavikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe mkoani Lindi. Sherehe hizo zilifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Elimu Nachingwea tarehe 18.3.2015 7Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi na wana vikundi vya WAMA katika Mradi wa Mwanamke Mwezeshe katika sherehe za kutimiza mwaka kwa vikundi hivyo zilizofanyika Nachingwea tarehe 18.3.2015.
10Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akimkabidhi cheti kwa Bi Fatuma Mchia, Mwenyekiti wa Umoja wa Vikundi vya WAMA Kwenye Mradi wa Mwanamke Mwezeshe kwa kuvuka lengo kwa kuingiza wanavikundi wengi kwenye mradi huo.
11Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akianzisha mchango wa papo kwa papo kwa ajili ya Mradi wa Mwanamke Mwezeshe na kufanikiwsa kukusanya zaidi ya shilingi milioni moja.
12Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanachuo wanaosomea ualimu kwenye Chuo cha Ualimu Nachingwea mara baada ya kuhudhuria sherehe za kutimiza mwaka kwa vikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe zilizofanyia chuoni hapo tarehe 18.3.2015.
14Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,CCM, Mama Salma Kikwete akishiriki katika mkutano wa ndani wa Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa akitokes Nachingwea ambako alihudhuria sherehe za kutimiza mwaka kwa vikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe tarehe b18.3.2015.
16Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM,Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Mnacho katika Wilaya ya Ruangwa ambao walijikusanya kwa wingi hadi kupelekea Mama Salma kusimama na kuzungumza nao. Mama Salma Kikwete yupo mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku tano.
17Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mnacho iliyoko wilayani Ruangwa. Mama Salma alikwenda shuleni hapo kukabidhi madawati 100 aliyowaahidi wakati alipozuru shule hiyo mwaka jana.
18Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikabidhi madawati 100 kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa Ndugu Sahius Kilowoko (kushoto) ambaye naye alimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Nicholaus Kombe (kulia). Mama Salma alitoa madawati hayo kwa Shule ya Msingi Mnacho iliyoko wilayani `humo tarehe 18.3.2015

Tuesday, 17 March 2015

MAONESHO YA KIMATAIFA YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA 2014, WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya MwafrikaWahimizwa kuonyesha bidhaa zenye viwango On 14:00 by Boniventura Fedinandi No comments WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yatakayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Novemba 16 hadi 23 wametakiwa kuonyesha bidhaa bora ambazo zitaleta ushindani katika soko la Tiba Asili. Maonyesho hayo yanafanyika nchini kwa mara ya kwanza na kuandaliwa na Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kushirikiana, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE). Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonyesho hayo, Boniventure Mwalongo alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa maonyesho hayo yanatoa fursa kwa wadau mbalimbali wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kuonyesha bidhaa zenye viwango kama mwanzo wa kupeana changamoto lakini pia kudhihirisha ubora wa bidhaa za Tiba Asili na Tiba Mbadala. “Tunaka kuona bidhaa zenye ubora kuanzia katika ufungashaji, maelekezo sahihi kuhusu matumizi lakini pia bidhaa hizo ziwe zinafaa kwa matumizi ya binadamu ikiwa ni pamoja na kuwa na viwango vinavyotakiwa,” alisema Mwalongo. Mwalongo alichukua fursa hiyo kuwaomba Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoa taarifa ya maonyesho hayo kwa waratibu wa mikoa na wilaya ili nao waweze kuwataarifu watabibu wa Tiba Asili na Mbadala waliosajiliwa katika maeneo yao ili waweze kushiriki kirahisi katika maonyesho hayo. “Njia hii itakuwa bora zaidi kwasababu itawarahishishia washiriki kupata fomu kutoka kwa waratibu wao wa wilaya au mkoa ambao pia wanawatambua kisheria,” alisema Mwalongo. Washiriki katika maonyesho hayo ni pamoja na Watabibu wa Tiba Asili, Watengenezaji wa Dawa Asili, Wakunga wa Tiba Asili, Kampuni za Dawa Asili na vipodozi vya dawa asili, Wasambazaji wa Vifaa vya Tiba Asili na Tiba Mbadala, Watengenezaji wa vyakula asili, kliniki za tiba asili na Tiba Mbadala. Aidha kuna taratibu nyingine za kuyashirikisha mashirika mengine ya kibiashara, taasisi binafsi za za serikali ili kutoa nafasi ya kutangaza biashara zao kupitia maonyesho hayo ambayo yatashirikisha wadau wa Tida Asili na Tiba Mbadala kutoka ndani na nje ya nchi. Kwa mujibu wa Mwalongo, hadi sasa kuna baadhi ya kampuni na taasisi ambazo zimeonyesha mwelekeo wa kutaka kudhamini maonyesho hayo na kuwa taarifa rasmi itatolewa baada ya kufikia makubaliano. Mbali na kutangaza Tiba Mbadala na Tiba Asili kwa mapana yake, Mwalongo alisema kuwa wanataka kujenga mtandao mkubwa wa kibiashara katika huduma ya Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa nchi za Afrika.

Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt

TIBA ASILI IMEGUBIKWA NA CHANGAMOTO

 AGOSTI 31 mwaka huu kulikuwa na Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yaliyofanyika Zanzibar katika viwanja vya Bustani ya Victoria mjini humo.
Moja ya mambo yaliyosisitizwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein, kupitia hotuba yake iliyosomwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ni pamoja na kukemea baadhi ya watu kisiwani humo wanaojitangaza kupitia baadhi ya misikiti na mabaraza kuwa wana uwezo wa kutoa Tiba Asili, akisema kufanya hivyo ni kinyume na sheria.


Lakini pia hakusita kusema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalipa kipaumbele suala la utafiti wa Tiba Asili na kuwa kuna uhusiano mzuri kati ya Wizara ya Afya na chama cha Watabibu Asili visiwani humo. Mwisho akaagiza mamlaka husika kushughulikia tatizo hilo.

Caroline mtafiti  wa tiba Asili kutoka chuo kikuu cha Berlin Ujerumani akipata maelezo kutoka kwa Mtabibu na Mtafiti wa Tiba Asili Bwana Boniventura Mwalongo ambaye pia ni Katibu wa ASSOCIATION OF TRADITIONA AND ALTERNATIVE MEDICINE IN EAST AFRIKA kutoka Tanzania  
Awali akisoma hotuba yake katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Zanzibar, Mayassa Salum Ally Alisema kuwa Wizara ya Afya kupitia baraza hilo imefanya jitihada mbali mbali kuinua Tiba Asili na Tiba Mbadala na kufanikiwa kuongeza idadi ya wataalamu hao ambapo sasa kuna watabibu 193 waliosajiliwa na kuna jumla ya kliniki 18 na vilinge  125.

 Rais wa chama cha Tiba Asili na Tiba Mbadala Afrika Mashariki Lyidia Matoke Akitoa Maelezo kuhusu Tiba Asili Kwa Makamu wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad

Sera ya Taifa ya Afya inaonyesha kuwa kabla ya Uhuru, huduma za afya zilikuwa zikitolewa zaidi katika maeneo ya shughuli za kiuchumi kama miji na mashanba makubwa. Baada ya Uhuru serikali iliweka msukumo zaidi katika kupanua huduma za afya ili kuwafikia wananchi walio wengi, hasa walioko maeneo ya vijijini.
Tiba Asili na Tiba Mbadala imekuwa ikishika kasi kila kukicha, japokuwa kuna changamoto za hapa na pale. Kuna haja ya kukubali kuwa changamoto nyingi zinazotokea katika eneo hili la Tiba Asili na Tiba Mbadala huenda zinatokana na ukosefu wa elimu ya kutosha kwa watanzania walio wengi ambao mara nyingi wamekuwa wakishindwa kutofautisha Tiba Asili na tiba nyingine zinazotolewa kwa kisingizio cha mtindo huo.
Kutokana na mkanganyiko huu, kumekuwa na tafsri za aina tofauti juu ya aina za waganga. Katika imani za kawaida, kuna aina tatu za waganga: Waganga wa Asili, Waganga wa Jadi na Waganga wa Kienyeji.
Kutokana na tafsiri inayotolewa na Chama Cha Utabibu Asili Tanzania (ATME),  Mganga wa asili ni yule anaye shughulika na tiba za maradhi kwa kutumia dawa za asili, kutibu maradhi  kwa binadamu, wanyama mimea kwa kufuata maadili ya utoaji huduma ya matibabu
Mganga wa Jadi: Anatumia Mila na Desturi katika tiba na utoaji dawa kwa wagonjwa iwe binadamu, wanyama, mimea. Hutegemea zaidi mila na desturi pamoja na tiba asili na dawa za asili kama kanuni na maadili ya utoaji huduma ya tiba.

Mganga wa kienyeji: Hana mafunzo maalumu ya tiba ya upande wowote wa tiba katika utoaji wake wa huduma kwa jamii. Ni mtu anayeweza kuchanganya taaluma mbalimbali hata za kisayansi ili mradi afanikishe alichokusudia. Mganga huyo pia anaweza kutumia vazi lolote liwe la Sheikh, Askofu, Daktari, Mganga wa Asili, ilimradi afikie lengo lake.

ATME wanasisitiza kuwa, mganga yoyote mwenye fani nzuri akiitumia katika kutenda maovu, huyo ndiye mganga wa kienyeji na wala si mtaalamu wa Tiba za Asili.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), takribani 60% ya wananchi huanza kutumia tiba asilia wanapopatwa na maradhi kabla ya kwenda vituo vya kutolea huduma za afya.
Nchini Tanzania Tiba Asili imekuwa na changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni ile ya baadhi ya watu kuihusisha na vitendo vya kishirikina, hali ambayo ni kinyume na sheria na taratibu zake, lakini pia kupotosha jamii.
Kwa mujibu wa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ya mwaka 2002, watabibu wote wa Tiba Asilia na Mbadala wako chini ya Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ambalo mbali na majukumu mengine lina jukumu la kusajili watabibu wote wenye sifa zinazotakiwa baada ya kuwafanyia usaili. Lakini pia kuendeleza na kuboresha huduma hiyo.
Moja ya mikakati ya Baraza hilo kwasasa ni kuhakikisha kuhakikisha kuwa watabibu wote wa Tiba Asili wanapata usajili, ili kudhibiti vitendo vinavyotishia maisha ya binadamu ambavyo vimekuwa vikihusishwa na Tiba Asili.
Baraza linakiri kuwa ni kweli kuwa kuna idadi kubwa ya watu anbao wanajihusisha na huduma ya tiba asili kinyemela, kitu ambacho ni kinyume na sheria. 
Katika semina ya vyombo vya habari iliyoandaliwa na ATME jijini Dar es Salaam Mei 15 mwaka huu katika Ukumbi wa NMR Dar es Salaam,  Mlezi wa chama hicho, Kingunge Ngombale Mwiru alisema Watanzania wengi ni wazito  kukubaliana na Tiba Asili, hali ambayo alisema inachangiwa na dhana ya kutawaliwa na wakoloni.
Mwenyekiti wa ATME Simba Abdulhamani Simba anasema kuna umuhimu wa serikali kuhakikisha kuwa watabibu wote wa tiba asili wanasajiliwa ili kupunguza matukio ambayo yamekuwa yakifanywa na baadhi ya watu wanaojiita wataalamu  wa tiba, lakini kwa kuichanganya na vitendo vya kishirikina.
Boninventure Mwalongo ni Mkurugenzi wa Kliniki ya Tiba Asili ya Boresa ya jijini Dar es Salaam ambaye pia ni Mratibu wa ATME, anasema kuwa kwa sasa wako katika mkakati wa kuhakikisha wanawashirikisha wadau mbalimbali ili jamii itambue umuhimu

wa tiba asili, ikiwa ni pamoja na kutoa semina kwa wadau mbalimbali.

Mwalongo anasema kuwa jambo jingine ambalo linatakiwa kudhibitiwa ni matangazo holela ya waganga ambayo yamekuwa yakibadikwa na hata mengine kutumika katika vyombo vya habari bila kufuata utaratibu.
Aidha kumekuwa na uhusiano wa karibu kati ya wadau wa Tiba Asili na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA). Mwaka 2012 kulikuwa na mkutano wa wadau wa dawa za asili. Halikadhalika Novemba 5 mwaka jana TFDA walikutana tena na wadau wa Tiba Asili.
Moja ya malengo ya mkutano huo ilikuwa ni pamoja na kukumbushana matakwa ya sheria pamoja na changamoto za udhibiti. Katika Mkutano huoMkurugenzi Mkuu waTFDA, Hiiti Sillo alisema kuwa moja ya changamoto katika Tiba Asili na Tiba Mbadala ni kuwepo katika soko bila kufuata taratibu za utengenezaji, lakini pia akasema akaongelea juu ya baadhi ya watu kutoa matangazo katika vyombo vya habari pasipo vibali vya Mamlaka hiyo.
Mwalongo anasema kuwa mikutano kama hiyo inadhihirisha jinsi Tiba Asili inavyozidi kupata uigo na kuzidi kuthaminiwa na kwamba watanzania wanapata mwanga zaidi wa kutambua kilicho bora na kuepuka udanganyifu kwa baadhi ya watu wanaojiita watabibu asili kinyume na utaratibu.
“Kwa ushirikiano kama huu nafikiri tutafika mahala watanzania walio wengi watafahamu umuhimu wa Tiba Asili kama ilivyo katika nchi za India na China ambako kwa mujibu wa takwimu za nchi hizo asilimia 80 za raia katika nchi hizo wanategemea Tiba Asili.
Ends.

Thursday, 12 March 2015

ELIMU KWA JAMII JUU YA AINA ZA WAGANGA

Katika swala la utoaji elimu kwa Jamii, elimu juu ya Tiba Asili inafaa itolewe na Waganga wa Asili wenyewe ili kuweza kubadilisha Imani zinazowapotosha wanajamii hata kufikia kutendeana maovu yanayopelekea mauaji. Elimu hii si vyema ikatolewa na Watu wengine kama Vile Maaskofu, Masheikh, Wanasheria, Madaktari wa Kisasa, Wanasiasa n.k kwa kuwa Jamii haitapokea ujumbe wao Kirahisi kwani wamezoeleka kwa Kazi zingine siyo kwa Kazi hiyo ya Imani za ushirikina na uchawi
Katika Imani ya kawaida Kuna Aina za waganga kama ifuatavyo
                              I.            Waganga wa Asili
                           II.            Waganga wa Jadi
                        III.            Waganga wa Kienyeji

1.    WAGANGA WA ASILI.
Mganga wa Asili ni yule anayeshughurika na Tiba za Maradhi kwa Kutumia dawa zaAsili ili kuondoa Maradhi yanayosumbua Jamii iwe kwa Binadamu, wanyama, mimea n.k kwa Kufuata maadili ya utoaji huduma ya Utabibu

2.    WAGANGA WA JADI.
Mganga wa Jadi ni yule anaetumia Mila na Desturi katika Tiba na Utoaji wa dawa kwa wagonjwa iwe Binadamu, Wanyama, Mimea n.k. hivyo hutegemea Zaidi Mila na Desturi kama kanuni na maadili ya utoaji wa Huduma ya Tiba.

3.    MGANGA WA KIENYEJI.
Mganga wa Kienyeji ni Yule Ambaye hana Mafunzo Maalum ya Tiba ya Upande wowote maalum wa tiba  ya Upande wowote katika utoaji wake huduma kwa jamii. Ni mtu anayeweza kuchanganya taaluma mbalimbali hata za kisayansi ili mradi afanikishe alichokusudia. Mganga huyo pia anaweza kutumia vazi lolote liwe la sheikh, askofu, daktari, Mganga wa asili n.k ili mradi atimize alokusudia. Mganga yeyote mwenye fani nzuri akiitumia katika kutenda maovu hufahamika kama mganga wa Kienyeji katika Tiba za Asili.

je Huyu ni Aina gani ya Mganga?

WATAALAMU WA TIBA ASILI WAKUTANA CHINI YA JUKWAA MOJA; WAONYESHA UMAHIRI KATIKA TIBA ASILI NA MBADALA

Mratibu wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania, Boniventura F. Mwalongo akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja yalikofanyika Maonyesho ya Tiba Asili na Mbadala


Dr. Jumanne wa Huduma ya Uponyaji akimsikiliza mmoja wa waliotembelea Banda lake kwenye Maonyesho ya Tiba za Asili na Mbadala katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Tiba  zinazotolewa na Dk. Jumanne ni zile zinazotokana na Matunda na Mboga Mbalmbali . Simu 0755087303





Dk. Salimu akiwaeleza watu waliofika kwenye maonyesho ya dawa asili jinsi dawa zake zinavyofanya kazi katika viwanja vya Mnazi Mmoja


Dk.Ahmad Darusi Salimu Mkurugenzi wa M. M.D.K Clinic akitoa maelezo ya jinsi dawa zake zinavyotakiwa kutumika. Yeye amebobea katika kutibu Kansa za aina zote na pia anayo dawa inayosaidia kuondoa magonjwa nyemelezi kwa wagonjwa wa UKIMWI. Simu 0754467406, 0787467406

Mkurugenzi wa Kampuniya Dk.Fadhili Herbal Medicine & Nutritional,akitoa maelezo kwa wateja ((hawapo pichani) waliofika kwenye Banda lake wakati wa Maonyesho ya Tiba za Asili na Mbadala yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja hivi Karibuni.  Dk. Fadhili pia ni Mshauri wa Afya katika Kampuni ya BF SUMA kutoka Marekani inayojishuhulisha na usambazaji wa dawa zenye Virutubisho vinavyoweza kuongeza kinga ya mwili (CD4) kwa 100%, kurekebisha Sukari na zingine nyingi.  Simu 0713834556

Dk. Nyakubaho (katikati) Mkurugenzi wa Kikundi cha tiba Asili cha Nyakiziba Shunga Tradtional Clinic. Wanazo dawa nyingi za kutibu maradhi mbalimbali kama inavyoonekana Pichani. Simu 0784936177, 0755570321

Bi EmilianaKokuhumuliza, Mtabibu wa asili anayetibu kwa kutumia mitishamba kutoka Mkoa wa Kagera. anapatikana Mjini Morogoro. Simu 0766903297. Picha zote na Muchunguzi Kamugisha wa ZUNGU

mhe.Kingunge Ngombale Mwilu akitembelea moja ya mabanda katika maonesho ya kwanza ya kimataifa ya tiba asili ya mwafrika

























































NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA

Flag Counter

Text Widget