MAONESHO YA KIMATAIFA
YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA 2014, WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara
ya Kimataifa ya Tiba Asili ya MwafrikaWahimizwa kuonyesha bidhaa zenye
viwango
On 14:00 by Boniventura Fedinandi No comments
WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya
Mwafrika yatakayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Novemba 16 hadi 23 wametakiwa kuonyesha bidhaa bora ambazo zitaleta
ushindani katika soko la Tiba Asili.
Maonyesho hayo yanafanyika nchini kwa mara ya kwanza na kuandaliwa na
Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kushirikiana, Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonyesho hayo, Boniventure
Mwalongo alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa maonyesho hayo yanatoa
fursa kwa wadau mbalimbali wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kuonyesha
bidhaa zenye viwango kama mwanzo wa kupeana changamoto lakini pia
kudhihirisha ubora wa bidhaa za Tiba Asili na Tiba Mbadala.
“Tunaka kuona bidhaa zenye ubora kuanzia katika ufungashaji, maelekezo
sahihi kuhusu matumizi lakini pia bidhaa hizo ziwe zinafaa kwa matumizi
ya binadamu ikiwa ni pamoja na kuwa na viwango vinavyotakiwa,” alisema
Mwalongo.
Mwalongo alichukua fursa hiyo kuwaomba Baraza la Tiba Asili na Tiba
Mbadala kutoa taarifa ya maonyesho hayo kwa waratibu wa mikoa na wilaya
ili nao waweze kuwataarifu watabibu wa Tiba Asili na Mbadala
waliosajiliwa katika maeneo yao ili waweze kushiriki kirahisi katika
maonyesho hayo.
“Njia hii itakuwa bora zaidi kwasababu itawarahishishia washiriki kupata
fomu kutoka kwa waratibu wao wa wilaya au mkoa ambao pia wanawatambua
kisheria,” alisema Mwalongo.
Washiriki katika maonyesho hayo ni pamoja na Watabibu wa Tiba Asili,
Watengenezaji wa Dawa Asili, Wakunga wa Tiba Asili, Kampuni za Dawa
Asili na vipodozi vya dawa asili, Wasambazaji wa Vifaa vya Tiba Asili na
Tiba Mbadala, Watengenezaji wa vyakula asili, kliniki za tiba asili na
Tiba Mbadala.
Aidha kuna taratibu nyingine za kuyashirikisha mashirika mengine ya
kibiashara, taasisi binafsi za za serikali ili kutoa nafasi ya kutangaza
biashara zao kupitia maonyesho hayo ambayo yatashirikisha wadau wa Tida
Asili na Tiba Mbadala kutoka ndani na nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Mwalongo, hadi sasa kuna baadhi ya kampuni na taasisi
ambazo zimeonyesha mwelekeo wa kutaka kudhamini maonyesho hayo na kuwa
taarifa rasmi itatolewa baada ya kufikia makubaliano.
Mbali na kutangaza Tiba Mbadala na Tiba Asili kwa mapana yake, Mwalongo
alisema kuwa wanataka kujenga mtandao mkubwa wa kibiashara katika huduma
ya Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa nchi za Afrika.
Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt
Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt
0 comments:
Post a Comment