ELIMU KWA JAMII JUU YA AINA ZA WAGANGA
Katika
swala la utoaji elimu kwa Jamii, elimu juu ya Tiba Asili inafaa itolewe
na Waganga wa Asili wenyewe ili kuweza kubadilisha Imani
zinazowapotosha wanajamii hata kufikia kutendeana maovu yanayopelekea
mauaji. Elimu hii si vyema ikatolewa na Watu wengine kama Vile Maaskofu,
Masheikh, Wanasheria, Madaktari wa Kisasa, Wanasiasa n.k kwa kuwa Jamii
haitapokea ujumbe wao Kirahisi kwani wamezoeleka kwa Kazi zingine siyo
kwa Kazi hiyo ya Imani za ushirikina na uchawi
Katika Imani ya kawaida Kuna Aina za waganga kama ifuatavyo
I. Waganga wa Asili
II. Waganga wa Jadi
III. Waganga wa Kienyeji
1. WAGANGA WA ASILI.
Mganga
wa Asili ni yule anayeshughurika na Tiba za Maradhi kwa Kutumia dawa
zaAsili ili kuondoa Maradhi yanayosumbua Jamii iwe kwa Binadamu,
wanyama, mimea n.k kwa Kufuata maadili ya utoaji huduma ya Utabibu
2. WAGANGA WA JADI.
Mganga
wa Jadi ni yule anaetumia Mila na Desturi katika Tiba na Utoaji wa dawa
kwa wagonjwa iwe Binadamu, Wanyama, Mimea n.k. hivyo hutegemea Zaidi
Mila na Desturi kama kanuni na maadili ya utoaji wa Huduma ya Tiba.
3. MGANGA WA KIENYEJI.
Mganga
wa Kienyeji ni Yule Ambaye hana Mafunzo Maalum ya Tiba ya Upande wowote
maalum wa tiba ya Upande wowote katika utoaji wake huduma kwa jamii.
Ni mtu anayeweza kuchanganya taaluma mbalimbali hata za kisayansi ili
mradi afanikishe alichokusudia. Mganga huyo pia anaweza kutumia vazi
lolote liwe la sheikh, askofu, daktari, Mganga wa asili n.k ili mradi
atimize alokusudia. Mganga yeyote mwenye fani nzuri akiitumia katika
kutenda maovu hufahamika kama mganga wa Kienyeji katika Tiba za Asili.
je Huyu ni Aina gani ya Mganga?
0 comments:
Post a Comment